Ofisi ya simu yashambuliwa Nigeria

Imebadilishwa: 22 Disemba, 2012 - Saa 14:44 GMT

Shambulio la kujitolea mhanga limefanywa kwenye ofisi ya kampuni ya simu za mkononi katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeriua.

Mwanamke atumia simu ya mkononi uwanja wa ndege wa Kano

Polisi wanasema mshambuliaji aliyejitolea mhanga, alisukumiza gari lake wenye ofisi ya kampuni ya Airtel.

Taarifa zinasema kampuni nyengine piya ililengwa.

Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo.

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, ambalo limekuwa likifanya mashambulio kwa miaka kadha kaskazini mwa Nigeria, limewahi kulenga makampuni ya simu za mkononi likisema kuwa kampuni hizo zinasaidia askari wa usalama kuwakamata wapiganaji.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.