Upinzani Misri utaendelea na mapambano

Imebadilishwa: 23 Disemba, 2012 - Saa 13:41 GMT

Chama kikuu cha upinzani cha Misri kinasema kitapinga matokeo ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya.

Upinzani nchini Misri

National Salvation Front inasema kuwa kura ya maoni - ambayo inaelekea kukubali kwa 60% katiba iliyopendekezwa na chama cha Muslim Brotherhood - iliingia dosari kwa sababu ya udanganyifu.

Chama hicho kimesema kura hiyo ya maoni siyo mwisho na mapambano yataendelea.

Kura ya maoni imezidisha mgawanyiko nchini Misri kati ya wafuasi wa Rais Morsi na chama chake cha Muslim Brotherhood upande mmoja na upinzani wa mrengo wa wastani upande wa pili.

Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema Wamisri wengi wamechoka na msukosuko wa kisiasa na pengine waliamua kutoshiriki kwenye kura.

Waliojitokeza kupiga kura walikuwa 30% tu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.