United yaponea chupu chupu City yalemewa

Imebadilishwa: 26 Disemba, 2012 - Saa 17:22 GMT
Jonny Evans

Jonny Evans akisherehekea bao lake

Manchester United, imeendelea uongozi wake katika ligi kuu ya England hadi alama saba mbele ya mabingwa watetezi Manchester City, baada ya kuilaza Newcastle 4-3.

James Perch, aliifungia newcastle bao la kwanza kabla ya Jonny Evans kusawazisha.

Hata hivyo Evans aligeuka na kuwa muasi pale alipofunga lango lao na kuipa Newcastle, uingozi kwa mara nyingine.

United ilijikakamua na Patrice Evra, akaifungia bao la pili.

Wageni wa United, hawakusitisha mashambulizi yao na dakika chache baadaye na kwa mara ya tatu katika mechi hiyo Newcastle, ilichukua uongozi kupitia kwa Papiss Cisse.

Baada ya kufungwa bao la tatu, United ilifanya mabadiliko machache na Nyota wake Robin Van Persie akainusuru meli ya United kuzama na kuifungia bao la tatu.

Huku mechi hiyo ikionekana, kuisha timu hizo mbili zikitoshana nguvu, Javier Hernandez alivurumisha kombora kali ambalo kipa wa Newcastle, hakuliona na kuipa ushindi Manchester United wa mabao 4-3.

Nusura United iandishe matokeo kama ya mwaka uliopita pale walioshindwa katika mechi yao ya siku kama ya leo.

Mabingwa watetezi sawa na mwaka uliopita walishindwa baada ya kulazwa kwa bao moja kwa bila na Sunderland.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.