Rais Zuma matatani kuhusu madai ya Mbwa

Imebadilishwa: 27 Disemba, 2012 - Saa 17:40 GMT
Rais Jacob Zuma

Rais JJacob Zuma akicheza dansi

Serikali ya Afrika Kusini, imeelezea matamshi yaliyotolewa na rais wa nchi hiyo, ambayo yamewakasirisha watu wanaopenda mbwa.

Rais Zuma, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema umiliki wa mbwa ni itikadi za wazungu na sio mila na desturi ya waafrika.

Lakini msemaji wa rais huyo amesema, rais Zuma, alikuwa akionya watu kutowashughulikia zaidi wanyama kuluko binadamu wenzao na hakupendekeza au uashiria mbwa kutupwa.

Amesema ujumbe huo ulikuwa na ni\ ya kuhimiza raia kuimarisha utamdani wa kiafrika na kuondoa imani na fikra za kikoloni.

Gazeti la Mercury nchini humo limeripoti kuwa rais Zuma, aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara katika mkoa wa KwaZulu Natal kuwa watu wanaotumia pesa kununu mbwa, kuwapeleka hospitalini na kutembea nao, ni watu wanaoiga na kufuata maadili ya wazungu.

Gazeti hilo liliendelea kunadi kuwa rais Zuma alisema kuwa vijana wa taifa hilo wanajaribu kuiga mfumo wa maisha wa makabila mengine yasiyo ya Kiafrika.

'' Hata ukipata nywele zako mafuta ya aina gani, huwezi kuwa mzungu'' Gazeti hilo lilimnukuu rais Zuma.

Matamshi yake yamewagadhabisha watu wengi nchini humo ambao wamechapisha hisia zao katika ukarasa mbali mbali za mitandao ya kijamii.

Wanaharakati wanaotetea maslahi ya wanyama wameshutumu kwa kutoa matamshi ambayo hayapaswi kutolewa na kiongozi wa nchi huku wengine wametuhumu na ubaguzi wa rangi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.