Waasi wa CAR wakataa pendekezo la rais Bozize

Imebadilishwa: 31 Disemba, 2012 - Saa 12:06 GMT

Rais wa CAR akiwahutubia wanainchi mjini Bangui

Waasi nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wamekaribia mji mkuu wa nchini Bangui na wamepuuzilia mbali, tangazo la rais wa nchini hiyo Francois Bozize, siku ya Jumapili, kuanzisha mazungumzo ya amani na viongozi wao.

Msemaji wa waasi wa Eric Massi, ameiambia BBC kuwa, ni vigumu sana kwao kumuamini rais Bozize, kwa sababu wanajeshi wake wanaendelea na harakati za kuwashambulia wapiganaji wao mjini Bangui.

Amesema, ikiwa jeshi la kutunza amani la Muungano wa Afrika , halitatumwa mjini Bangui, waasi hao wataingia na kutoa ulinzi wa wafuasi wao.

Lakini serikali ya nchi hiyo imekanusha madai hayo, ya kuwafanya mashambulio dhidi ya wafuasi wa waasi hao.

Siku ya Jumapili, rais Bozizi alitangaza kuwa yuko tayari kuunda serikali ya muungano wa kitaifa na waasi hao na kuwa hatawania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2016.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.