Pauni ya Misri yasambaratika

Imebadilishwa: 31 Disemba, 2012 - Saa 12:31 GMT

Sarafu ya Misri

Rais wa Misri, Mohammed Morsi, amesema kuwa hababaishwi na hatua ya sarafu ya taifa hilo kushuka dhamana kwa kiwango kikubwa.

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali MENA, limemnukuu rais Morsi akisema kuwa hali itaimarika katika siku kadhaa.

Matamshi yake yanakuja huku benki kuu ikizindua mfumo wa ubadilishanaji wa pesa za kigeni kwa mnada miongoni mwa benki za taifa hilo ili kujaribu kuthibiti thamani ya pauni ya Misri.

Wamisri wengi wamekuwa wakibadilisha pesa zao kwa dola ya marekani wakihofia kuwa thamani ya pauni itashuka.

Bwana Morsi ameapa kukabiliana na matatizo hayo ya kiuchumi lakini wachambuzi wanasema raia wengi hawaamini iwapo ataweza kufanya hivyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.