Siku 3 za maombolezi yangazwa Ivory Coast

Imebadilishwa: 2 Januari, 2013 - Saa 13:35 GMT

Nguo na viatu za wakati wa msongamano nchini Ivory Coast

Serikali ya Ivory Coast imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa baada ya zaidi ya watu sitini kuuwawa na wengine wengi kujeruhiwa kwa kukanyagwa wakati wa onyesho la fataki kuukaribisha mwaka mpya katika mji mkuu wa Abidjan.

Maafisa wanasema wengi wa waathiriwa waliokufa ni vijana.

Kuna ripoti za kutatanisha kuhusu kilichosababisha maafa hayo karibu na uwanja wa michezo uliopo mjini Abidjan.

Baadhi ya wale walioshuhudia kisa hicho wanasema watu waliingiwa na wasiwasi baada ya vijana waliokuwa wamejihami kwa visu kuanza kuiba simu za mkononi huku wengine wakisema ni utepetevu wa maafisa wa usalama katika kuthibiti umati.

Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouatarra, amewatembelea hosipitalini baadhi ya wale waliojeruhiwa na kusema kuwa kutakuwa na uchunguzi kuhusiana na kisa hicho ambacho alikitaja kuwa mkasa wa kitaifa.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.