UN yataka wapiganaji watoke mijini

Imebadilishwa: 5 Januari, 2013 - Saa 14:43 GMT
Wanajeshi wa serikali wakilinda mji wa Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataiafa limetoa wito kwa kundi la wapiganaji katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wasiingie mji mkuu, Bangui, na watoke katika miji waliyoiteka.

Baraza la Usalama limewataka wapiganaji hao washiriki katika mazungumzo ya amani yatayoanza nchini Gabon juma lijalo.

Wapiganaji hao ambao walikaribia mji mkuu wa Bangui hivi karibuni wanataka rais wa jamhuri hiyo ya Afrika ya Kati, Francois Bozize, ajiuzulu.

Jamhuri ya afrika ya Kati ni moja kati ya nchi maskini kabisa barani Afrika na imepita kwenye mizozo mingi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.