Jeshi lakabiliana na waasi Mali

Imebadilishwa: 8 Januari, 2013 - Saa 10:00 GMT

Wapiganaji wa Tuareg na wale wa kiisilamu wanakabiliana na jeshi la Afrika linalosaidia Mali

Wanajeshi wa Mali wamekabiliana na wapiganaji wa kiisilamu katika eneo la Kati mwa nchi.

Kwa mujibu wa duru za kijeshi, ni makabiliano ya kwanza ya aina yake kutokea kati ya pande hizo mbili tangu wapiganaji wa kiisilamu pamoja na waasi wa Tuareg kuteka eneo la Kaskazini mwa nchi Aprili mwaka jana.

Wapiganaji hao waliripotiwa kupiga hatua katika kukaribia eneo la Kusini mwa nchi ambalo linadhibitiwa na serikali.

Kwa sasa haijulikani ikiwa kulikuwa na majeruhi wowote.

Jeshi lilitumia zana nzito dhidi ya wapiganaji hao katika kijiji cha Gnimignama.

"wapiganaji hao wa kiisilamu , sasa wako katika maeneo ya mpakani kwenye msitari wa mbele wa vita. Eneo la kwanza kutoka mpaka wa Mauritania na Magharibi katika eneo la Douentza,'' alisema waziri wa ulinzi wa Mali kanali Yamoussa Camara.

Waakilishi wa serikali ya Mali pamoja na wapiganaji hao wakiwemo wale wa Tuareg wanatarajiwa kufanya mazungumzo katika nchi jirani ya Burkina Faso tarehe kumi mwezi Januari.

Wapiganaji wa kiisilamu wanadhibiti eneo la Kaskazini mwa Mali

Waasi waliteka eneo la Kaskazini baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi.

Ushirikiano kati ya wapiganaji hao wa kiisilamu na Tuareg ulivunjika huku wapiganaji wakitwa maeneo ya mijini.

Waasi hao wameharibu madhabahu katika mji wa Timbuktu na kuweka sheria kali ya kiisilamu hali iliyosababisha ghadhabu katika nchi za kimataifa.

Mwezi jana baraza la usalama la umoja wa mataifa, liliunga mkono jeshi la pamoja la nchi za Afrika kusaidia serikali ya Mali kutwa eneo la Kaskazini kutoka kwa waasi kwa njia salama katika miezi kadhaa inayokuja.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.