'Ndege zisizo na rubani kutumiwa DRC'

Imebadilishwa: 9 Januari, 2013 - Saa 08:32 GMT

Marekani hutumia ndege hizi kupambana na wanamgambo Pakistan

Mkuu wa kitengo cha umoja wa mataifa cha kulinda amani ametoa wito wa kutumiwa ndege zisizo na rubani aina ya Drones kufanyia uchunguzi katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, kama njia moja ya kuleta amani nchini humo.

Herve Ladsous amesema kuwa ndege hizo zitasaidia wanajeshi elfu kumi na saba wanaolinda amani kutoa ulinzi kwa raia nchini humo.

Lakini balozi wa umoja wa mataifa wa Rwanda alisema kuwa serikali yake ina wasiwasi kuhusu matumizi ya ndege hizo.

Rwanda ilikanusha madai ya kuunga mkono kundi la waasi wa m23 mashariki mwa congo

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.