Mchanga wa Sierra Leone watoka wapi?

Imebadilishwa: 9 Januari, 2013 - Saa 10:40 GMT

Sira Leone sand land

  • Nchi ambayo ingali na makovu ya vita vibaya vya wenyewe kwa wenyewe, Sierra Leone, ilitabiriwa kuwa moja ya nchi ambazo zingekuwa kwa kasi kubwa mwaka 2012. Lakini kando na ukuwaji wake, pia inashuhudia ukuwaji wa miundo msingi, ikiwemo barabara, na majengo mengine yanayojitokeza katika maeneo ya mijini.
  • Lakinin ujenzi unakuja na gharama yake, mchanga unaohitajika sana. Na je unatoka wapi? katika fuo za bahari ya nchi hiyo.
  • Athari zimeanza kujitokeza kwani bahari inaendelea kukosa msingi wa kuilinda ikiwa ni mchanga huo ambao unatwaliwa kila kukicha kulingana na halmashauri ya mazingira
  • Katika kijiji cha Lakka mjini Freetown, majengo ya kale yanaendelea kuporomoka na ndio urembo uliosalia kando ya bahari. Jengo hili liliharibiwa mwaka 2004, kufuatia mmomonyoko wa mchanga baada ya sehemu hii ya bahari kuwa mojawapo ya maeneo ambako mchanga unakusnaywa sana.
  • Sehemu hii ya bahari inajulikana kama Hamilton ambako mchanga huchimbwa siku mbili kwa wiki, zaidi ya lori 40 hufika hapa kubeba mchanga huo.
  • Mama huyu ni mkaazi wa eneo la Hamilton na anaelewa kuwa makaazi yake siku moja yatakuja kuwa historia au yataathirika kutokana na mmomonyoko wa mchanga. "nina wasiwasi mkubwa kuhusu makaazi yangu, lakini siwezi kumudu bei ya kuhamia kwingineko'' anasema
  • Zaidi ya miaka kumi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuisha, Sierra Leone hatimaye inatumai idadi kubwa ya watalii waliokuwa wanazuru nchi hiyo miaka ya nyuma wataweza kurejea. Uchimbaji wa mchanga ni tisho kwa utalii.
  • Uchimbaji huo unapswa kuwekewa vikwazo yani watu wachimbe tu katika sehemu moja kwa wakati mmoja lakini kuna hofu watu hawatii vikwazo. Wakati mwingine watu huchimba nyakati za usiku.
  • Jamii za pwani zimegawanyika kuhusiana na uchimbaji hasa kwa sababu vijana wasio na kazi hijupatia riziki yao kwa njia hii.
  • Kwa nchi yenye asilimia sabini ya vijana wasio na kazi, wachimbaji wanasema ni jukumu la serikali kuwapa ajira

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.