Kesi dhidi ya Mubarak kusikilizwa upya

Imebadilishwa: 14 Januari, 2013 - Saa 08:45 GMT
Mubarak alipofikishwa mahakamani mwaka 2011

Rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak, ameruhusiwa kufanyiwa kesi nyengine kwa makosa ya kutozuwia mauaji ya waandamanaji mamia kadha wakati wa ghasia zilizomuondoa madarakani.

Mahakama ya rufaa mjini Cairo, baada ya kikao kifupi, ilitoa amri hiyo ya Bwana Mubarak kufanyiwa kesi nyengine.

Mwezi wa Juni mahakama ilitoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa Rais Mubarak kwa hatia ya kuwa na dhamana ya mauaji ya waandamanaji yaliyofanywa na askari wa usalama ambao wakijaribu kuzima ghasia za mwaka wa 2011.

Mkuu wa usalama wa Bwana Mubarak, Habib el-Adly, ambaye anatumikia kifungo cha maisha kwa mashtaka kama hayo, piya atafanyiwa kesi nyengine.

Mubarak, anayesalia kizimbani,pia atafunguliwa kesi nyingine ya ufisadi ammayo ilifutiliwa mbali mwezi Juni kwa kukosa ushahdi wa kutosha.

Alitawala Misri kwa miaka 30 akiponea jaribio la mauaji dhidi yake kabla ya mapinduzi ya kiraia dhidi ya utawala wake.

Mohammed Morsi wa chama cha Muslim Brotherhood alichaguliwa kama rais kwenye uchaguzi uliofanywa mwezi Juni mwaka jana.

Jaji Ahmed Ali Abdel Rahman alitangaza kuwa mahakama imeamua kukubali rufaa ya mshtakiwa na hivyo kuamuru kesi kusikilizwa tena.

Mmoja wa mawakili wa Mubarak, aliambia vyombo vya habari kuwa kesi hiyo itasikiloizwa tena kwa misingi ya ushahidi uliotolewa kwenye kesi ya kwanza.

"hakuna ushahidi wowote mya utaruhusiwa kutolewa katika kesi hiyo,'' alisema jaji

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.