Mahujaji waogelea katika mto Ganges India

Imebadilishwa: 14 Januari, 2013 - Saa 10:06 GMT

Mamilioni wanatarajiwa kuogelea kwenye mto huop mwishoni mwa leo

Maelfu ya watu wamekuwa wakioga katika makutano ya mito miwili ya Ganjes na Yauna eneo la Allahabad nchini India.

Ni katika siku ya kwanza ya tamasha la Kumbh Mela.

Takriban mahujaji milioni kumi wanatarajiwa kuogelea katika mtu huo hadi kufikia mwishoni mwa leo.

Tamasha hili ambalo hufanyika kila baada ya miaka kumi na miwili, ni mojawapo ya mikusnayiko mikubwa ya watu duniani. Zaidi ya watu milioni 100, wanatarajiwa kuhudhuria tamasha hilo litakalodumu miaka 55

Waumini wa dini ya Hindu wanaamini kuwa wakiogelea katika mto huo , dhambi zao zitafutika na kisha itawasaidia kupata msamaha na kuokoka kutokana na dhambi.

Mnamo mwaka 2001, zaidi ya watu milioni 40 walikusanyika katika siku rasmi ya kuogelea kwenye mto huo na kuvunja rekodi ya idadi kubwa ya watu kuwahi kukusanyika katika sehemu moja duniani.

Wahindi wanaamini kuwa asali ilianguka kwenye mto huo kufuatia vita kati ya miungu na mashetani waliokuwa wanaipigania, na baada ya hapo imekuwa desturi ya wahindi kuogelea kwenye mto huo.

Waumini waliomba wakati wakioga katika makutano ya mito hiyo miwili ya Yamuna na Ganges kuanzia hapo jana.

Mji wa Allahabad umekuwa ukijiandaa kwa tamasha hilo kwa miezi mingi na watu wameweka mahema kuuzingira mto wenyewe.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.