Waziri mkuu wa Pakistan kukamatwa

Imebadilishwa: 15 Januari, 2013 - Saa 11:20 GMT

Wadadisi wanasema ilikuwa wazi utawala wa Pervez ungekumbwa na matatizo


Mahakama ya juu zaidi nchini Pakistan imeamuru kukamatwa kwa waziri mkuu wa nchi hiyo Raja Pervez Ashraf kufuatia madai ya ufisadi.

Bwana Ashraf anatuhumiwa kwa kupokea rushwa wakati alipoidhinisha miradi ya kuzalisha umeme alipokuwa waziri wa maji na kawi mwaka 2010.

Mahakama iliamuru kukamatwa kwa washukiwa wegine kumi na tano waliohusishwa na madai hayo.

Wadadisi wanasema hatua hiyo huenda isisababishe kuondolewa mamlakani mara moja kwa waziri mkuu huyo.

Hatua hii inakuja wakati muhubiri mashuhuri sana Tahirul Qadri alipowaongoza maelfu ya waandamanaji mjini Islamabad, akitaka viongozi wa serikali kujiuzulu.

Picha kwenye televisheini nchini humo zimeonyesha waandamanaji wakishangilia punde baada ya habari kutolewa kuwa mahakama imeamuru waziri mkuu akamatwe.

Mwandishi wa BBC nchini humo, anasema kuwa huenda ni jambo ambalo halikutarajiwa , lakini kwa wadadisi wengi hatua hii huenda ni ishara ya dalili ya madai kuwa muhubiri huyo anaungwa mkono na baadhi ya watu katika idara ya mahakama na jeshini.

Katika miaka ya hivi karibuni , serikali ya Pakistan , idara ya mahakama pamoja na baadhi ya maafisa wa jeshi wamekuwa wakilumbana.

Kiongozi aliyemtangulia bwana Ashraf, Yousuf Raza Gilani, alilazimika kuondoka mamlakani mwezi Juni mwaka jana babada ya mahakama kumpata na hatia ya kukosa kufuatilia kesi ya ufisadi, dhidi ya rais wa nchi hiyo.

Bwana Ashraf aliteuliwa katika nafasi hiyo lakini wadadisi wanasema kuwa utawala wake pia utagubikwa na matatizo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.