Polisi maalum wa Uingereza auawa Kenya

Imebadilishwa: 15 Januari, 2013 - Saa 13:17 GMT

Ramani ya Kenya

Mwanamume muingereza Aliyeuawa nchini Kenya siku ya Jumamosi alikuwa polisi maalum katika idara ya polisi wa Matropolitan nchini Uingereza.

Jamal Moghe,mwenye umri wa miaka 26, kutoka Wembley, Kaskazini mwa London, pia alifanya kazi kama mfanyakazi wa umma nchini Uingereza.

Inaaminika aliuawa na wezi wa mifugo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kuchangisha pesa za msaada.

Kamanda wa mtaa wa Ealing, Andy Rowell alisema kuwa : "tumeshtushwa sana na habari za kifo cha Jamal.''

Bwana Moghe alikuwa afisaa wa upelelezi katika mtaa wa Ealing na pia kufanya kazi kama afisaa maalum wa polisi katika mta alikoishi wa Brent.

Kamanda Rowell alisema kuwa alikuwa mwanachama kikosi cha Ealing na pia aliamua kuhudumia jamii yake kwa kujitolea kama afisaa maalum.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje nchini Uingereza, alithibitisha kifo cha Jamal na akakelezea kuwa wanatoa msaada kwa familia yake wakati huu mgumu.

Eneo la Kaskazini mwa Kenya ambalo linapakana na Ethiopia na Somalia, ni eneo tambarare na lisilokuwa na watu wengi na linakabiliwa na changamao ya kiusalama.

Wizi wa mifugo ni tatizo sugu katika eneo hilo, na mwaka jana pekee polisi kadhaa waliuawa katike eneo hilo na watu walioshukiwa kuwa wapiganaji kutoka Somalia.

Wapiganaji wa Al shabaab wameahidi kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kufuatia harakati za jeshi la Kenya dhidi yao mwezi Oktoba mwaka jana wakisaidiana na wanajeshi wa Somalia kuwaondoa wapiganaji hao kutoka Mogadishu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.