Mateka 30 wafanikiwa kutoroka Algeria

Imebadilishwa: 17 Januari, 2013 - Saa 12:11 GMT

Kiwanda cha mafuta ambako wafnyakazi wa kigeni wameshikwa mateka

Wafanyakazi 30 wa kigeni wamefanikiwa kutoroka kutoak kwa kiwanda cha gesui Mashariki mwa nchi hiyo ambako idadi kubwa ya wafanyakazi wakiwemo wa kigeni kutekwa nayara katika kiwanda hicho.

Wafanykazi hao waliuziliwa wapiganaji wa kiisilamu ambao ni tawi la Al qaeeda katika nchi za Maghreb siku ya Jumatano.

Hata hivyo shirika rasmi la habari la Algeria ambalo lilitoa taarifa hii, halikueleza namna ambayo wafnyakazi hao walifainikiwa kutoroka.

Wanajeshi wa nchi hiyo waliokuwa wanazingira kiwanda hicho, inaarifiwa walikabiliana na wanamgambo waliokuwa wamjihami wakati wa usiku.

Baadhi ya wafanyakazi hao wa kigeni, ni wafanyakazi wa shrika la mafuta la BP.

Katika taarifa ya shirika hilo, hali ilisemekana kuwa tete.

Wanajeshi wangali wanakizingira kiwanda hicho.

Wanamgambo hao, walivamia kiwanda hicho katika eneo la Amenas siku ya Jumatano baada ya kuwaua watu wawili mmoja raia wa Uingereza na mwingine wa nchi hiyo katika shambulzi dhidi ya basi.

Serikali inasema kuwa wafanyakazi kadhaa wa kigeni wamezuiliwa kama mateka ingawa wanamgambo hao wanasema idadi ya watu waliotekwa ni 41.

Mateka hao ni pamoja na raia wa Uingereza , Japan , Marekani , Ufaransa na raia wa Norway

Taarifa moja inayosemekana kutoka kwa wanamgambo hao, ilikuwa na madai ya kutaka Ufaransa kukoma harakati zake za kijeshi dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali.

'Mpaka wafungwa'

Waziri wa mambo ya ndani Daho Ould Kabila alisema kuwa wanamgambo hao walitaka kuondoka nchini humo na mateka wao lakini akawazuia kuondoka.

"hatuko tayari kufanya mashauriano na kundi hilo'' waziri huyo aliambia waandishi wa habari.

Bwana Kabila aliongeza kuwa wanamgambo hao ni raia wa Algeria na wanapokea amri zao kutoka kwa Mokhtar Belmokhtar, kamanda mkuu wa al-Qaeda tawi la nchi za Maghreb.

Mwaka jana Belmokhtari aliunda kundi lake la kigaidi baada ya kukata uhusiano na viongozi wengine wa Al Qaeeda.

Raia hao waliteka katika kituo cha mafuta cha BP

Aidha Kabila alisema kuwa kundi lililojihami vikali, lilishambulia basi moja lililokuwa linawabeba wafanyakazi kutoka kiwanda cha Amenas nyakati za jioni.

Kiwanda hicho kinamilikiwa na kampuni ya serikali ya mafauta Sonatrach, pamoja na kampuni ya mafuta ya BP.

Kiko umbali wa kilomita 1,300 Kusini Mashariki mwa Algiers, na umbali wa kilomita 60 Magharibi mwa mpaka wa Libya.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.