Al Shabaab kumuua jasusi wa Ufaransa

Imebadilishwa: 16 Januari, 2013 - Saa 11:01 GMT

Ufaransa inaamini kuwa Denis Alex hayuko hai

Wanamgambo wa Al-Shabab nchini Somalia wanasema kuwa watamuua jasusi wa Ufaransa Denis Allex, ambaye Ufaransa ilisema kuwa alikuwa tayari ameuawa wakati jaribio la kumuokoa lilipotibuka.

Walisema kuwa Ufaransa inapaswa kulaumiwa ikiwa atauawa. Na pia inapaswa kulaumiwa kwa mauaji ya makomando wengine wawili waliouawa Ijumaa katika msako uliofanywa mjini Bulo Marer.

Maafisa nchini Ufaransa wanasema kuwa waliamini bwana Allex alikuwa ameuawa na mateka wake wakati wa jaribio la kumuokoa ingawa al-Shabab wanasema hakuwepo hapo wakati huo.

Hakuna thibitisho lolote la kifo chake limetolewa hadharani.

Al-Shabab imetuma picha ya mwili wa komando mmoja, aliyeuawa lakinin sio wa Allex, jina la kikazi la jasusi huyo ambaye amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya miaka mitatu.

Katika ujumbe wao kupitia Twitter, al-Shabab walisema ufaransa ndiyo imesababisha kuuawa kwa Alex kwa sababu ya njama yao ya kutaka kumuokoa.

Waziri wa ulinzi aliambia idhaa ya redio ya ufaransa, kuwa anaamiini Alex ameuawa tayari, na kuituhumu Al Shabaab kwa kuchzea hisiasa za watu.

Al Shabaab

Ufaransa inasema kwamba makombando wa Ufaransa waliwaua wanamgambo 17 Ijumaa. Walioshuhudia makabiuliano hayo wanasema kuwa raia kadhaa pia walifariki kwenye makabiliano hayo.

Waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian, alisema Ufaransa ilichukua hatua kwa sababu ya kile ilichosema ni madai ya kupuuzi yaliyokuwa yanatolewa na Al-Shabab.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.