Wanajeshi tayari kwa vita vya ardhini Mali

Imebadilishwa: 17 Januari, 2013 - Saa 06:43 GMT

Wanajeshi wa Ufaransa

Wanajeshi wa Ufaransa wanajiandaa kwa makabiliano yao ya kwanza muhumi ya ardhini wa wapiganaji wa waasi nchini Mali, baada ya kuanza safari hiyo kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Bamako.

Msafara wa magari ya kivita 30 yaliondoka mjini Diabaly, takriban kilomita 350, Kaskazini mwa mji mkuu, mji ambao ulitekwa na wapiganaji hao waasi siku ya Jumatatu.

Kikosi cha kwanza cha wanajeshi wa Muungano wa Afrika, kinatarajiwa kuwasili baadaye hii leo, ili kuyasaidia wanajeshi hao wa Ufaransa.

Ufaransa iliingilia kati mzozo huo siku ya Ijumaa ili kuzuia wapiganaji hao wa waasi kuingia mji mkuu.

Wapiganaji hao wa Waasi ambao wamejawa na matumaini waliingia mjini Diabaly siku ya jumatatu, na kutwaa uthibiti wake kutoka kwa wanajeshi wa serikali.

Mashambulio ya Anga

Wanajeshi wa Ufaransa wanasema waasi wangali wanaudhibiti mji wa Konna

Wanaanga wa Ufaransa tayari wamefanya mashambulio kadhaa ya anga dhidi ya vituo muhimu vya waasi hao.

Mkuu wa Majeshi wa Ufaransa Edouard Guillaud amesema wanajeshi wake tayari wameanzisha mashambulio ya ardhini.

Wanajeshi hao wanaelekea Kaskazini wakiwa na mitutu ya bunduki tayari kwa makabiliano.

Kwa wakati mmoja watu walisimamisha msafara huo na kuwapungia mikono wanajeshi hao wa Ufaransa.

Hadi kufikia sasa juhudi za ufaransa dhidi ya waasi hao zimeimarishwa kwa mashamulizi ya ndege za kivita na helikopta.

Hata hivyo hatua hiyo hainaonekani kuzaa matunda kwani kungekuwa na mafanikio tu endapo mabomu hayo yanayorushwa yangekuwa yakiwalenga waasi wanaohusika kwani kwa sasa wana uwezo wa kujipanga upya.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa msafara huo utavamia miji ya Diabalay ama Konna ambayo inakaliwa na wapiganaji wa kiislamu.

Nani anauthbiti mji wa Kona?

Raia wa Mali wakiwakaribisha wanajeshi wa Ufaransa

Wakati Ufaransa ilipoanza kuwashambulia wapiganaji hao Mashariki mwa Mali, ilisemekana kuwa mamia ya wanajeshi wa Ufaransa walikuwa wakishiriki.

Wakati huohuo, maafisa katika jeshi la Ufaransa, wamekanusha madai yaliyotolewa awali na jeshi la Mali, kuwa wameweza kuudhibiti mji wa Konna uliokuwa umetekwa na waasi.

Ufaransa, ilianza harakati zake za kijeshi kusaidia jeshi la Mali dhidi ya waasi Ijumaa iliyopita baada ya wapiganaji wa kiisilamu kuuteka mji wa Konna na kuanza kuukaribia mji mkuu.

Mji mwingine wa Kati ,Diabaly, ulitekwa na waasi Jumatatu iliyopita.

Wanajeshi wa Ufaransa wakishirikiana na wa Mali, wameanza kuelekea katika mji huo kuanza operesheni yao ya ardhini dhidi ya waasi.

Mwezi Machi mwaka jana wapiganaji wa kiisilamu wakishirikiana na waasi wa Tauareg, waliteka Kaskazini mwa Mali.

Hivi karibuni wapiganaji hao walio na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda, walidhibiti eneo hilo na kuanza kuweka sheria kali za kiisilamu.

Pindi mpango wa serikali wa kuutwaa mji huo , waasi nao wakaanza kuelekea Kusini mwa nchi.

Rais Francois Hollande

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, alisema kuwa Ufaransa ina lengo moja tu, kuhakikisha inaondoka Mali, baada ya nchi hiyo kuwa salama na kuhakikisha kuwa hakuna tisho lengine la kigaidi dhidi ya nchi hiyo.

Mashambulio ya Anga

Hatua ya wanajeshi kuteka mji muhimu wa Konna wiki jana , ndiyo ilichochea Ufaransa kuchukua hatua za kijeshi kusaidia Mali.

Ndege za Ufaransa, zilianza kufanya mashambuliziya angani dhidi ya wapiganaji hao siku iliyofuata hadi Jumamosi.

Maafisa walisema kuwa jeshi la Mali lilisema limeweza kudhibiti mji wa Konna na kwamba wapiganaji
100 waliuawa.

Lakini waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian, aliambia waandishi wa habari mjini Paris kuwa mji huo bado uko mikononi mwa waasi.

Ndege za kijeshi za mali ziliweza kuzuia waasi waliokuwa wameingia eneo lililo katikati mwa miji ya Douentza na Gao.

Duru hata hivyo zinaarifu kuwa jeshi la Mali halina uwezo mkubwa wa kudhibiti waasi kivyao

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.