Avamiwa na Kifaru mbugani Afrika Kusini

Imebadilishwa: 16 Januari, 2013 - Saa 09:20 GMT

Mwanamke aliyevamiwa na Kifaru mbugani Afrika Kusini

Mwanamke mwenye umri wa miaka 24 amejeruhiwa vibaya baada ya kuvamiwa na Kifaru saa chache baada ya kupiga picha ya mnyama huyo nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la Beeld, Chantal Beyer alipata majeraha ya mapafu na ubavu wake baada ya kuvamiwa na mnyama huyo katika mbuga ya wanyama ya Aloe Ridge umbali wa kilomita 40 kutoka mjini Johannesburg.

Bi Beyer,mwanafunzi wa chuo kikuu cha West Rand,alikuwa na mumewe pamoja na watalii wengine wakivinjari mbuga hiyo na kupiga picha na wanyama hao. Muda mfupi baadaye ndipo akavamiwa

Anasemekana kuwa katika hali mbaya ingawa madaktari wameweza kuidhibiti.

Thuluthi moja ya vifaru wote duniani wako Afrika Kusini ikikisiwa kuwa takriban vifaru,28,000.

Lakini nchi hiyo imeshuhudia ongezeko la visa vya uwindaji haramu huku biashara ya pembe za wanyama hao zikinawiri hasa barani Asia. Wengi wanaamini kuwa pembe hizo zina uwezo wa kuponya.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.