Tevez apigwa marufuku kuendesha gari

Imebadilishwa: 16 Januari, 2013 - Saa 13:35 GMT

Carols Tevez

Mshambulizi wa Manchester City, Carlos Tevez, amepigwa marufuku ua kuendesha gari kwa muda wa miezi sita ijayo, baada ya kupatikana na hatia ya kutojibu barua zilizotumwa kwake na polisi, kuhusiana na mashtaka ya kuendesha gari kwa mwendo wa kasi zaidi.

Tevez, 28, amekanusha madai kuwa ndiye aliyekuwa akiliendesha gari hilo wakati, camera za polisi zilipoinasa kuwa inakwenda kwa kasi.

Akijitetea, Tevez alisema kuwa hakutambua barua hizo zilikuwa zikitoka kwa polisi kwa kuwa hakufahamu maana ya nene "constabulary".

Mchezaji huyo kutoka Argentina, alikiri mashtaka mawili mbele ya hakimu mkuu mkaasi wa Manchester ya kutotoa habari kwa polisi.

Tevez pia alipigwa faini na kuamrishwa kulipa gharama za keshi ambazop kwa ujumla ni pauni elfu moja mia tano na hamsini.

Wakili wa Tevez, Gwyn Lewis, alifahamisha mahakama hiyo kuwa mteja wake anaelewa maana neno polisi na kusema kwamba Tevez haelewi maana ya neno gumu kama vile Constabulary.

Wakili huyo alisema barua hiyo iliandikiwa imetoka Cheshire Constabulary na kwamba hakuna neno polisi hata moja.

Machi 28 mwaka uliopita, Tevez alipatikana na hatia ya kutotoa habari kwa polisi wakati gari lake liliponaswa likiendeshwa klwa mwendo wa kasi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.