Mashambulizi ya kushangaza Garissa Kenya

Imebadilishwa: 17 Januari, 2013 - Saa 12:34 GMT

Takriban watu watano waliuawa Jumatano na wengine wanne kujeruhiwa katika ufyatuaji risasi katika mkahawa mmoja mjini Garissa Kaskazini mwa Kenya.

Kulingana na taarifa ya polisi katika eneo hilo, wapiganaji wa kiisilamu wa Al Shabaab ndio waliohusika na shambulizi hilo.

Afisaa mmoja mkuu wa magereza ni miongoni mwa waliofariki.

Wanajeshi kadhaa na polisi wameuawa mjini Garissa katika miezi ya hivi karibuni.

Al-Shabab wametishia kulipiza kisasi kwa jeshi la Kenya kwa kuunga mkono serikali ya Somalia dhidi yao

Watu waliokuwa wamejihami walivamia jengo moja na kufyatua risasi usiku wa kuamkia leo, kulingana na gazeti la Standard.

Watu watatu waliuawa papo hapo na wengine kufariki wakipelekwa hospitalini.

Polisi Kaskazini mwa Kenya wako macho kufuatia taarifa kuwa makundi ya wanamgambo kutoka Somalia yamevuka na kuingia Kenya.

Mwezi Oktoba mwaka jana, watu waliokuwa wamejihami, walimuua polisi mmoja kwa kumpiga risasi huku wakimjeruhi mwingine.

Mmashambulizi kadhaa yamekuwa yakifanya mjini Garissa na watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Al Shabaab

Mwezi Uliofuata wa Novembe, wanAjeshi watatu wa Kenya na polisi wawili pia waliuawa kwa kupigwa risasi.

Mashambulizi mengine ya hivi karibuni, yaliyohusisha Al-Shabab mjini Nairobi yaliwaacha watu wengine 15 wakiwa wamekufa na hivyo kuchochea hali ya wasiwasi kati ya jamii ya wasomali na wakenya .

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.