Jeshi la Mali laukomboa mji wa Konna

Imebadilishwa: 18 Januari, 2013 - Saa 15:00 GMT

Wanajeshi wa Mali

Jeshi la Mali limefanikiwa kuukomboa mji wa Konna uliokuwa umetekwa na waasi nchini Mali .

Hii ni baada ya wapiganaji hao kutoroka kulingana na taarifa za wenyeji katika mjui huo

Ufaransa ilianza harakati zke kusaidia jeshi la Mali wiki moja iliyopita kwa sababu ya hatua ya waasi kuuteka mji huo wa Kaskazini.

Mapema wiki hii, maafisa wa Ufaransa, walikanusha madai ya jeshi kuwa m,ajeshi ya Mali yalikuwa ymeukomboa mji wa Konna.

Wakati huohuo, shirika la Umoja wa Matifa la kuwahdumia wakimbizi, limeelezea hofu kuwa mapigano hayo huenda yakawalzimisha watu laki saba kutoroka makwao.

Takriban watu 150,000 tayari wamekimbilia nchi jirani.

Duru zinasema kuwa shirika la UNHCR, limeelezea kuwa watyu zaidi huenda wakatoroka Mali huku wengine 300,000 wakiacha bila makao.

Kikosi cha kwanza cha wanajeshi wa Afrika, kinachojiunga na muungano wa wanajeshi wa kimataifa dhidi wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali, kiliwasili nchini humo usiku wa kuamkia leo.

Hali ya Mali inaendelea kudhihirika huku nchi baada ya nyingine zikiendelea kujitolea kutuma vikosi.

Ufaransa tayari ambayo Mali ilikuwa chini ya ukoloni wake, ndiyo inaongoza harakati hizo Kaskazini mwa nchi.

Inatumia ndege za kijeshi pamoja na vifaru ambavyo vinashambulia maeneo ya waasi hao kote Kaskazini mwa Mali na maeneo mengine ya jangwa la Sahara.

Ufaransa ilianza kwa kutuma wanajeshi zaidi ya miamoja Mali lakini siku kadhaa tu katika harakati hizo, ikaahidi kuongeza idadi hiyo hadi wanajeshi elfu mbili na miatano.

Jeshi la Mali ambalo limesmekana kutokuwa na uwezo mkubwa

Katika tukio lengine, nchi kubwa zaidi Magharibi mwa Afrika Nigeria, nayo pia ikajitolea kutuma wanajeshi,miasita. Idadi hiyo sasa imeongezeka mara dufu.

Nchi za Magharibi sasa kila kukicha zinakumbana na wapiganaji wenye nguvu wa kiisilamu katika msitari wa mbele nchini Mali.

Lakini kupambana na wanamgambo sio kazi rahisi. Wanaelewa vyema maeneo ya jangwa kuliko wanajeshi wa kigeni.

Pia wana miungano kadhaa au kuungwa mkono na wapiganaji wengine upande wa pili wa jangwa katika miji mikuu ya nchi jirani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.