Magaidi walaumiwa kwa vifo vya Wangereza

Imebadilishwa: 20 Januari, 2013 - Saa 12:22 GMT

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, amesema imethibitishwa kuwa wananchi watatu wa Uingereza ni kati ya mateka waliouwawa nchini Algeria.

Kinu cha gesi cha In Amenas, Algeria

Alisema wanaobeba dhamana ya vifo hivyo ni watekaji nyara.

Bwana Cameron alisema shambulio hilo katika jangwa la Algeria linakumbusha ulimwengu juu ya tishio la ugaidi katika Afrika Kaskazini na duniani.

Waziri wa habari wa Algeria alisema mateka kama 23 wamekufa na kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Piya alisema wapiganaji 32 waliouliwa na jeshi walitoka nchi sita tofauti, za Kiarabu, Afrika na kwengineko.

Wakaazi wa mji wa In Amenas ambako kisa hicho kimetokea wana wasi-wasi kuwa tukio katika kinu kilioko hapo litaathiri vibaya uchumi wa eneo hilo:

"Hii inatuathiri sisi kwa sababu ya mafuta, hili ni tete.

Watu wamekuja hapa kufanya kazi siyo kufanya ghasia.

Hili ni eneo la salama na ikiwa ugaidi utabaki hapa, basi hili eneo litakuwa si kitu.

Hili ni eneo tete lenye mafuta na gesi, na watu wengi wameuwawa"

Mwengine alisema:

"Nafikiri sasa makampuni yote ya Kifaransa yanataka kuondoka na hivo kutakuwa hakuna kazi.

Hilo ndio tatizo.

Tulikuwa na kazi na kila kitu kilikuwa sawa.

Lakini baada ya haya yaliyotokea..basi. kila kitu kitasimama.

Wengi watakosa kazi."

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.