Kampeini ya dharura dhidi ya Polio Misri

Imebadilishwa: 23 Januari, 2013 - Saa 15:30 GMT

Mtoto akipewa chanjo nchini Pakistan

Maafisa nchini Misri wanasema kuwa watafanya kampeini ya dharura ya kuwapa chanjo ya Polio watoto.

Hii ni baada ya ukaguzi kuonyesha kuwa virusi vya ugonjwa huo vilipatikana katika bomba la maji taka kutoka kwa sehemu moja iliyojaa watu mjini Cairo.

Hakuna yeyote aliyeonyesha dalili za kuathiriwa na homa hiyo, na hapajakuwa na visa vyovyote vya ugonjwa huo nchini Misri tangu mwaka 2004.

Shirika la afya duniani, linasema kuwa virusi vilivyogunduliwa vinafanana na vile vilivyopatikana Kusini mwa Pakistan.

Kampeini hiyo ya kuangamiza Polio, nchini Pakistan,zilisitishwa karibuni baada ya watu tisa waliohusika na kampeini hiyo kuuawa katika muda wa wiki moja, mwezi jana.

Kumekuwa na juhudi nyingi kutaka kumaliza Polio katika nchi tatu ambako ni kama janga ikiwemo Nigeria, Afghanistan, Nigeria na Pakistan.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.