Juhudi za kufuta sheria ya ubakaji Morocco

Imebadilishwa: 23 Januari, 2013 - Saa 15:14 GMT

Wanawake wanaopinga sheria hiyo wakisema inawakandamiza

Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake , wameipongeza hatua ya serikali kuahidi kufutilia mbali kipengee cha sheria ambacho kinawaruhusu wanaume wabakaji kukwepa jela kwa kuwaoa wale waliowabaka ,(waathriwa wa kitendo kile cha ubakaji).

Sheria hii hasa hasa inagusia wasichana walio na umri mdogo ambao sheria inasema wanaume waliowabaka waweze kuwaoa.

Lakini wanasema kuwa ni hatua ya kwanza tu katika kubadili sheria hiyo na kwamba haitoshi kukomesha dhulma dhidi ya wanawake nchini Morocco.

Hatua ya kushinikiza sheria hiyo kufutiliwa mbali, ilichukuliwa mwaka mmoja baada ya msichana mmoja mwenye umri wa miaka 16 Amina al-Filali, kujinyonga kwa kulazimishwa kuolewa na mtu aliyekuwa amembaka.

Mtu huyo alitumia kipengee hicho ambacho kinaruhusu wale waliohukumiwa kwa kosa la ufisadi au utekaji nyara wa msichana mdogo kumuoa ili kukwepa kifungo jela.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.