Kenya haitazungumza na Al Shabaab

Imebadilishwa: 24 Januari, 2013 - Saa 16:28 GMT

Silaha ambazo jeshi la Kenya lilinasa kutoka kwa Al Shabaab

Serikali ya Kenya imeshutumu tishio la magaidi wa Al shabaab walio nchini Somalia la kutaka kuwaua Wakenya wanaowazuilia iwapo matakwa yao hayatasikilizwa na serikali hiyo.

Wanataka wapiganaji wa kiisilamu wanaozuiliwa nchini humo kwa madai ya kuhusika na vitendo vya kigaidi kuachiliwa.

Aidha imesema kuwa haiko tayari kwa mazungumzo yoyote na wapiganaji hao walio na uhusiano na kundi la Al Qaeeda

Jeshi la Kenya limetaja vitisho hivyo kama kitendo cha kigaidi kwa kuwa waliotekwa ni wafanyakazi wa kutoa huduma za kimisaada na wala sio wanajeshi.

Al shabaab walitoa kanda ya video ya wakenya wawili waliowateka nyara mwaka mmoja uliopita na kusema kuwa watawaua ikiwa Kenya haitawaachilia wafungwa hao.

Wiki moja iliyopita wapiganaji hao walimuua jasusi mmoja wa Ufaransa Denis Allex kulipiza kisasi hatua ya Ufaransa kuwakandamiza waisilamu na kwa harakati zao za kijeshi nchini Mali.

Wapiganaji wa Al Shabaab wakiwa mazoezini

Kanali Cyrus Oguna, msemaji wa jeshi la Kenya , ambalo limekuwa likipambana na wapiganaji hao nchini Somalia, tangu mwaka 2011, alisema kuwa mateka walioonyeshwa kwenye kanda hiyo ya video sio wafungwa wa kivita kwa sababu hawakuwahi kupigana jeshini.

Alisema Serikali haiwezi kufanya mazungumzo na kundi la kigaidi. Kile ambacho Al Shabaab inafanya ni kitendo cha uhalifu ambacho kinapaswa kuadhibiwa .Alisema kuwa wanapaswa tu kuwaachilia.

Wawili hao walitekwa nyara mwezi Januari wakati wanamgambo walipovuka mpaka na kuingia Kenya na kisha kushambulia kituo cha polisi mjini Wajir huku polisi kadhaa wakiuawa kwenye shambulizi hilo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.