Masaibu wa wakimbizi wa Syria

Imebadilishwa: 24 Januari, 2013 - Saa 16:04 GMT

Mkimbizi wa Syria

Umoja wa mataifa umeonya tena kuhusiana na janga la kibinadamu linalowakabili wakimbizi kutoka Syria.

Mshirikishi wa Umoja huo nchini Jordan, Andrew Harper, ameiambia BBC kwamba idadi ya wakimbizi wanaovuka mpaka kutoka Syria kila siku ni kati ya elfu mbili na tatu, huku wengine elfu sitini wakisubiri kuvuka mpaka.

Mwandishi wa BBC katika kambi kuu nchini Jordan amesema kuwa kumiminika kwa raia wa Syria nchini humo ni mzigo mkubwa kwa nchi hiyo na Umoja wa mataifa.

Kambi ya Zaatari tayari inatoa hifadhi kwa wakimbizi elfu sabini huku zaidi ya wakimbizi wengine elfu 25 wakiwa tayari wamewasili mwanzoni mwa mwa mwaka huu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.