Waingereza watakiwa waondoke Somaliland

Imebadilishwa: 27 Januari, 2013 - Saa 17:26 GMT

Uingereza imewashauri wananchi wake waondoke Somaliland kwa sababu za usalama.

Ramani ya Somalia

Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Uingereza inasema kuna tishio maalumu linalowakabili watu kutoka mataifa ya magharibi walioko Somaliland na raia wa Uingereza wanafaa kuondoka haraka.

nafikiriwa kuwa kuna Waingereza wachache tu katika eneo hilo, wengi wao wafanyakazi wa mashirika ya misaada, lakini wengine wenye uraia wa Somalia na Uingereza wanasafiri baina ya Uingereza na Somaliland.

Siku kadha zilizopita, Uingereza na mataifa mengine ya Ulaya yalionya raia wake mjini Banghazi, Libya, kuhusu tishio linalowakabili.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.