Msaada wa kijeshi kwa Zimbabwe wasitishwa

Imebadilishwa: 28 Januari, 2013 - Saa 08:36 GMT

Mahakama nchini Afrika Kusini imesimamisha kwa muda kupelekwa kwa helikopta ilizokuwa imeliahidi jeshi la Zimbabwe. Hii ni kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za kibinadamu, AfriForum.

Shirika hilo lilitoa ombi la dharura la mchango huo kutoka Afrika Kusini wa helicopta za Alouette ambazo Afrika Kusini haitumii tena kuwa usitolewe tena.

lilisema kuwa kwamba ingekuwa si haki kulipa vifaa jeshi kama la Zimbabwe, ambalo linaegemea upande wa serikali, wakati huu uchaguzi mkuu wa mwaka huu unapokaribia.

Wizara ya Ulinzi ya Afrika Kusini ilisema kwamba helikopta hizo hazitaundwa, bali tu zitatumika kwa vipuri vyake.

Vikwazo

Uchaguzi nchini Zimbabwe wa 2008 ulikumbwa na ghasia na madai ya ununuzi wa kura.

Wiki iliyopita, viongozi wa kisiasa nchini Zimbabwe ambao wamezozana kwa muda mrefu kususu katiba mpya, walikubaliana, jambo lililoondoa kikwazo kikubwa kilichokuwa kinakwamisha kupangwa kwa kufanyika kwa uchaguzi mwaka huu.

Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la kutetea haki za kibina damu la Human Rights Watch lilisema kwamba hadi sasa maafisa wa ulinzi wangali wanaiunga mkono kisiasa serikali pekee, huku wakiwa wandani wa Rais Mugabe na Zanu-PF badala ya kuwa jeshi la Wazimbabwe wote.

Muungano wa Nchi za Ulaya pia umeiwekea Zimbabwe vikwazo dhidi ya kununua au kuingiza silaha zozote.

Kwa mujibu wa AfriForum, helikopta hizo, zilizotengenezwa Ufaransa, zilitumiwa na serikali ya kibabe wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Angola katika miaka ya 1970 na 1980 ili kuwasaidia waasi wakati huo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.