Uingereza kushirikiana na Algeria kuisalama

Image caption Mateka 37 waliuawa nchini Algeria baada ya wanamgambo wa kiisilamu kuteka kiwanda cha gesi

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, ambaye yuko ziarani nchini Algeria, anasema nchi hizo mbili zimekubaliana kuanzisha ushirikiano mpya wa kukabiliana na tisho linalosababishwa na wanamgambo wa kiislamu walioko kote Kaskazini mwa Afrika.

Alikuwa akizungumza baada ya mazungumzo na rais wa Algeria Abdelmalek Sellal .

Ziara ya Bwana Cameron imefanyika wiki mbili baada ya mateka 37 wa kigeni kuuwawa na wanamgambo waliokuwa wamewateka nyara katika kiwanda cha gesi katika jangwa la Algeria.

Katika ziara hiyo ameambatana na mkuu wa ujasusi wa kigeni M-I-6.

Mwandishi wa BBCmjini Algiers anasema ushirikiano wa kijasusi ni suala litakalopewa kipaumbele katika ushirikiano huo, lakini masuala kama usalama wa mipaka na usfiri wa anga pia yatajumuishwa.