Askofu mkuu mpya wa Kianglikana aapishwa rasmi

Askofu wa zamani wa Durham Justin Welby atakuwa askofu mkuu wa 105 wa Canterbury katika ibada itakayofanyika katika kanisa kuu la St Paul's Cathedral hii leo, baada ya kupitishwa kisheria na tume ya uteuzi iliyomchagua mwaka jana.

Askofu Welby anachukua nafasi ya Dr Rowan Williams, ambaye aliondoka madarakani mwishoni mwa mwezi wa Desemba na kuchukua nafasi ya uongozi wa chuo cha Magdalene cha Cambridge.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya kidini Robert Pigott anasema kuwa , zilizokuwa ni taratibu za kisheria tu sasa zimegeuka kuwa sherehe za ibada ya kanisa kwa kiongozi mpya wa kanisa la England.

Iwe kwa kiwango na kiroho kuidhinishwa kwa kutawazwa kwa askofu mkuu wa Canterbury' ni tukio la kipekee.

Maaskofu wakuu watakuwa katika kanisa la St Paul huku mahakama ya sheria ikitumiwa kufafanua lugha tamu kuelezea cheo atakachokuwa nacho Justin Welby katika wadhfa wake mpya. Sherehe na cheo hicho hubadilishwa baada ya karne kadhaa .

Sherehe nyingine za kuvutia kwa ajili ya Askofu Webly zinazotarajiwa kupambwa na muziki maalum wa kanisa hilo zitafanyika mwezi ujao katika kanisa kuu la Canterbury .

Hata hivyo , Justin Welby aliomba kuwa sherehe za leo zifanyike kwa ibada kamili , zikiwemo nyimbo za ibada , ili kuonyesha umuhimu wa kidini wa sherehe za kutawazwa kwake kwa kiti hicho kipya .

Wakati askofu mkuu wa York John Sentamu atakapokuwa akisoma na kuweka ishara za kutawazwa kwake, askofu Welby atakuwa askofu mkuu wa , na kiongozi wa kiroho wa waumini wapatao milioni moja wa kanisa la kianglikana duniani