Washukiwa wa M23 wakamatwa Afrika Kusini

Polisi nchini Afrika Kusini wamewakamata watu wanaoaminika kuwa washukiwa wa kundi la waasi wa M23 wanaoendeshea harakati zao katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Polisi wanasema kuwa wamewazuilia katika mkoa wa Lompopo Kaskazini mwa nchi.

Inaarifiwa walikamatwa na polisi wa kupambana na ugaidi baada ya kupokea habari katika operesheini iliyofanywa kwa miezi kadhaa.

Washukiwa hao, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baadaye leo.

Waasi wa M23 walianza harakati zao, Mashariki mwa DRC mwaka jana na kwa siku kadhaa kuuteka mji wa Goma , hatua iliyowalazimisha maelfu ya watu kutoroka makwao na kukimbilia usalama wao.