Wanawake 7 watalii wabakwa Mexico

Wanaume waliokuwa wamejihami wamewabaka wanawake saba watalii karibu na hoteli moja ya kitalii nchini Mexico ijulikanayo kama Acapulco.

Polisi wanasema kuwa wanaume hao waliokuwa wamejifunika nyuso zao, walivamia makaazi ya wanwake hao kkusini mwa mji mapema aasubuhi.

Sita kati ya wanawake hao ni raia wa Uhispania, wa saba akiwa raia wa Mexico.

Hii ni moja ya visa vibaya zaidi vya uhalifu wa kijinsia kuwahi kuripotiwa na kufanyika dhidi ya watalii tangu hali ya usalama kuanza kudorora mwaka .2006.

Hoteli ya Acapulco ni salama lakini magenge ya walanguzi wa madawa ya kulevya huendesha biashara zao hapo sawa na makundi mengine madogo ya wahalifu.