Mgawanyiko waibuka serikalini Tunisia

Image caption Inaarifgiwa polisi mmoja aliuawa kwenye maandamano hayo

Ripoti kutoka nchini Tunisia zinasema kuwa huenda kuktokea mgawanyiko katika chama tawala cha Ennadha.

Jambo hili linatokea baada ya tangazo la waziri mkuu kuwa anaunda serikali mpya itakayojumuisha wataalamu, kufuatia mauaji ya mawanasiasa mkuu wa upinzani.

Kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika chama tawala, Ennadha, Abdelhamid Jelassi, anasema kuwa waziri mkuu, Hamadi Jabali, hakushauriana na vyama vya muungano tawala kuhusu uamuzi wake.

Bwana Jelassi alisema kuwa mazungumzo yngali yanaendelea na vyama vingine kuhusu kuundwa lwa muungano mpya.

Hali ya msukosuko imekumba Tunisia baada ya mauaji ya kiongozi mmoja wa upinzani Shokri Belaid, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Ennahda.

Mauaji yake ndiyo yamesababisha maandamano dhidi ya serikali mjini Tunis na katika miji mingine mikubwa.

Kulikuwa na utulivu mjini Tunis, Tunisia usiku kucha baada ya siku moja ya vurugu kufuatia mauaji ya mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Shokri Belaid.

Waziri Mkuu wa Tunisia, Hamadi Jebali, alitangaza nia yake ya kuunda Serikali ya watalamu kufuatia mauaji ya Belaid.

Maelfi ya waandamanaji waliitaka serikali tawala kujiuzulu kuhusiana na mauaji hayo.

Lakini mmoja wa viongozi wa serikali alilaani mauaji hayo akiyataja kuwa kitendo cha uoga na kuwa wale waliomuua kiongozi huyo hawatafanikiwa kusababisha vurugu Tunisia.

Mauaji ya Bwana Belaidi, ambaye amekuwa mkosoaji mkuu wa Serikali yalisababaisha ghasia katika miji kadhaa nchini. Waandishi wa habari kutoka eneo hilo wanasema kufikia sasa afisaa mmoja wa polisi ameuliwa na waandamanaji hao.

Image caption Jamaa za marafiki za marehemu Shokri Belaid

Akihutubia taifa katika matangazo ya moja kwa moja katika runinga Bwana Jebali alisema kuwa Serikali hiyo itaendelea kwa muda bila mwelekeo wa vyama hadi Uchaguzi Mkuu utakapofanywa.

Maelfu ya waandamanaji walikuwa wametoa wito kujiuzulu kwa chama kinachotawala cha Kiislamu cha ENNAHDA kufuatia mauaji ya Belaid.

Muungano wa vyama vya kiraia uliokuwa mwanachama wa serikali ya muungano, uliondoka Serikalini na kuitisha mgomo wa taifa lote.