Nyama ya farasi madukani Uingereza

Image caption Nyama ya Farasi

Maafisa wa afya nchini Uingereza wameanza kugundua kiasi kikubwa cha nyama ya farasi inayouzwa kama nyama ya ngombe katika maduka makubwa.

Mikebe kadhaa ya nyama inayouzwa na kampuni ya vyakula ya FINDUS imethibitishwa kuwa na nyama ya farasi.

Shirika la Afya la kitaifa nchini humo limesema kuwa hakuna ushahidi iwapo chakula hicho ni hatari kwa afya ya mwanadamu lakini uchunguzi ungali unaendelea.

Shirika hilo linasema kuna hatari kuwa heunda kuna wahalifu wanaohusika katika kupakia nyama hiyo ya farasi kiharamu.

Mwezi uliopita nyama iliyodhaniwa kuwa ngombe ilibidi iondolewe kwenye maduka baada ya kuonekana kuwa ilikuwa imechanganyishwa na nyama ya farasi na nguruwe.