Dhoruba ya theluji yavuma Marekani

Malaki ya watu wa kaskazini-mashariki mwa Marekani wamekosa umeme huku dhoruba kali ya theluji inavuma kwa siku ya pili.

Theluji nyingi imemwagika na imefika kina cha mita moja na kukata umeme kwa nyumba zaidi ya nusu-milioni.

Kinu cha nishati cha nuklia kilioko Massachusetts ilibidi kufungwa na magari yamepigwa marufuku mabara-barani.

Majimbo matano ya mwambao wa mashariki yametangaza hali ya dharura, yaani Massachusetts, Rhode Island, Connecticut, New York na Maine, na wakaazi wameshauriwa kubaki majumbwani mwao.

Safari zote za ndege zimevunjwa na safari za treni piya zimesimamishwa.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema hii inaweza kuwa dhoruba kali kabisa kupiga New England kwa miongo kadha.