Uchaguzi wa Mali kufanyika Julai 7

Mali itafanya uchaguzi mkuu tarehe saba mwezi Julai. Tangazo hili limetolewa na serikali ya mpito.

Inatarajiwa kuwa hatua kubwa katika kuimarisha uthabiti wa Mali baada ya jeshi la Ufaransa kuisaidia kupambana na makundi ya wapiganaji Kaskazini mwa Nchi.

Uchaguzi wa wabunge nao utafanyika tarehe 21 mwezi Julai pamoja na duru ya pili ya uchaguzi ikiwa itahitajika.

Maelfu ya majeshi kutoka Ufaransa na Afrika wako nchini Mali.

Uchaguzi ulistahili kufanyika Aprili mwaka jana lakini baada ya mapinduzi ya kijeshi kufanyika , hali ikawa yenye utata nchini humo.

Jeshi lilisema kuwa lililazimika kuchukua hatua kwani halikuwa na uwezo mkubwa kukabiliana na uasi,ulioanza Januari Kaskazini mwa nchi.

Muungano wa wapiganaji wa Tuareg waliotaka kujitawala walitumia pengo la ukosefu wa usalama Mali na kuvuruga eneo la Kaskazini, sehemu ambayo ni kubwa hata kuliko Ufaransa.

Ufaransa iliamua kuchukua hatua mwezi jana kusaidia jeshi la Mali kupambana na wapiganaji na hadi kufika sasa wapiganaji wameweza kufurushwa kutoka miji mikubwa waliokuwa wameiteka