Wafuasi wa Ennahda waandamana Tunis

  • 16 Februari 2013

Maelfu ya wafuasi wa chama tawala cha Kiislamu cha Tunisia, Ennahda, wameandamana kupinga mpango wa waziri mkuu kuunda serikali ya wataalamu.

Waandamanaji walikusanyika kati ya mji wa Tunis kuunga mkono Ennahda na haki yake ya kuongoza nchi.

Waziri Mkuu Hamadi Jebali - wa pili kwa madaraka katika chama cha Ennahda - amependekeza iundwe serikali itayowakilisha wengi ili kupambana na msukosuko uliosababishwa na mauaji ya kiongozi wa upinzani, Chokri Belaid, awali mwezi huu.

Familia ya Bwana Belaid imekishutumu chama cha Ennahda kwamba kimechochea mauaji hayo.

Ennahda inakanusha tuhuma hizo.