Marehemu wakili afunguliwa kesi Urusi

Sergei Magnitsky
Image caption Kaburi la marehemu Sergei Magnitsky

Mahakama moja nchini Urusi imesikiza kesi ya matayarisho dhidi ya marehemu wakili aliyekuwa anapinga vikali ufisadi nchini humo. Marehemu Sergei Magnitsky, alifariki mwaka 2009.

Mahakama ilisema kwamba kesi itaanza tarehe 4 Machi. Inaaminika kwamba hii ndiyo mara ya kwanza katika historia ya Urusi kwa mshtakiwa kufunguliwa kesi baada ya kifo chake.

Bwana Magnitsky alikamatwa mnamo mwaka 2008 baada ya kuwalaumu maafisa kwa kufanya ulaghai katika utoaji wa kodi, ingawaje yeye mwenyewe baadaye alishutumiwa kwa kufanya vivyohivyo.

Kifo chake mwaka mmoja baadaye kilizua mzozo wa kidiplomasia kati ya Urusi na Marekani.

Mwaka ulipopita Marekani ilipitisha Sheria ya Magnitsky, inayowaweka watu wasiotakikanakwenye orodha maalum.Watu hao huwa ni wale ambao wanashukiwa kuwa wamekiuka haki za binadamu.

Kwa upanda wake, Rais Vladimir Putin wa Urusi alitia saini sheria ya kuwazuia Wamarekani kuwaasili mayatima Warusi.