Tashwishi kuhusu usalama wa mateka Nigeria

Waziri mmoja wa serikali ya Ufaransa aliyekuwa amesema kuwa familia iliyokuwa imetekwa na wanamgambo nchini Cameroon, ameelezea kutokuwa na uhakika.

Awali taarifa zilisema kuwa kuwa familia moja iliyokuwa imetekwa nyara Kaskazini mwa Cameroon mapema wiki hii wamepatikana wakiwa salama nchini Nigeria.

Familia hiyo inayojumuisha watoto wanne, wanasemekana kuachwa katika nyumba moja isiyotumika Dikwa.

Jamaa hao walitekwa nyara na watu waliokuwa wakiendesha pikipiki huku wakiwa wamejihami kwa bunduki.

Awali serikali ya Ufaransa ilidai kuwa familia hiyo ilikuwa imetekwa nyara na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram nchini Nigeria.

Serikali ya Ufaransa imetoa wito kwa raia wake kutozuru maeneo ya Kaskazini mwa Cameroon na katika mataifa ya Magharibi na Afrika ya kati kufuatia utekaji nyara huo.