Wagomea wajitetea vikali kwenye mjadala

Image caption Wagombea walihojiwa kuhusu swala tete la aradhi

Wagombea wanane wa urais nchini Kenya walikuwa na kibarua kigumu kujieleza kuhusu maswala tete kuhusiana na uchaguzi mkuu kwenye mjadala wa pili na wa mwisho kabla ya uchaguzi mkuu Jumatatu ijayo.

Uchaguzi unafanyika miaka mitano baada ya ule uliokumbwa na ghasia mwaka 2007-8.

Takriban watu 1,100 walifariki katika ghasia hizo, huku maelfu ya wengine wakiachwa bila makao.

Wagombea wakuu Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wakiwa katika msitari wa mbele kwenye kinyang'anyiro, wana ushawishi mkubwa katika uchaguzi wa tarehe nne.

Hata hivyo wadadisi wanasema kuwa wagombea wote wana ushawishi pia hususan ikiwa kutakuwa na duru ya pili.

Naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta ni mwanawe rais wa kwanza wa jamuhuri ya Kenya na yeye pamoja na mgombea mwenza wake William Ruto wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya kimataifa ya ICC baada ya kuhusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007.

Kenyatta, Odinga na wagombea wengine sita, walihojiwa katika mjadala huo uliovutia hisia kali kuhusu maswala ya ardhi, sheria za ajira, mageuzi ya ardhi, baadhi ya mswala muhimu yanyowagusa wakenya wengi.

Ardhi ni mojwapoa ya mambo yaliyosababisha ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007 katika eneo la Pwani, pamoja na mkoa wa Rift Valley, na liliibua hisia wakati wa mjadala.

Familia ya Kenyatta inamiliki sehemu kubwa ya ardhi nchini Kenya karibu hekari elfu laki tano kulingana na mashirika ya kijamii. Hata hivyo alisisitiza kuwa mashamba hayo yanamilikiwa kulingana na sheria za nchi.

Hata hivyo Raila alisisitiza kuwa huwezi kuruhusu mbwa mwitu kulinda mbuzi wako akiwa anagusia jibu alilotoa Kenyatta.

Huu ulikuwa mjadala wa pili na wa mwisho kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika Aprili nne na wadadisi wanasema ni idadi ndogo sana ya wakenya walioshawishiwa kupiga kura kwani tayari watu walifanya uamuzi wao kitambo sana.