Wauawa katika shambulizi la bomu Mali

Image caption Wapiganaji Mali

Zaidi ya watu saba wamefariki baada ya gari moja lililokuwa na bomu kulipuka Kidal nchini Mali.

Wanajeshi wa ufaransa wako Kidal kupambana na wapiganaji waislamu tangu mwezi ulopita.

Waasi wa Tuareg wanaunga mkono juhudi za ufaransa dhidi ya waasi wamesema kuwa mlipuaji huyo wa bomu alipitia katika moja ya vituo vya ukagazi.

Hili ni shambulio la pili huko Kidal chini ya wiki moja karibu na milima ya Ifogha inayotumika kuwa maficho ya wapiganaji.

Shambulio hilo linasemekana kulenga kizuizi cha polisi kilichokuwa kinalindwa na wapiganaji wa Tuareg ambao wamebatilisha msimamo wao na kuanza kuunga mkono jeshi la Ufaransa.

Wapiganaji wa kiisilamu walifurushwa kutoka Kidal na ngome zengine zao lakini wamekuwa wakiendelea kufanya uvamizi na kufanya mashambulizi ya bomu.

Afisaa mkuu wa misaada wa umoja wa mataifa, ameelezea kuwa maelfu ya watu wameachwa bila makao nchini Mali wakihofia hata kurejea walikotoka.

Zaidi ya watu 430,000 waliotoroka vita mwaka jana Kaskazini mwa Mali, hawakuhisi kuwa tayari kurejea nyumbani licha ya hali ya usalama kuimarika, alikariri John Ging,afisaa katika ofisi ya mratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.

Wale waliosalia walihofia kuwa mgogoro ungali kuisha na kuongeza huku kukiwa na ripoti za watu kukatwa mikono na miguu pamoja na kubakwa, jambo linalofanywa dhidi ya wanawake na watoto