Wagombea binafsi kufaidika Tunisia

Image caption Kumekuwa na ghasia nchini Tunisia kufuatia uamuzi wa serikali kuhusu nyadhifa za mawaziri

Kiongozi wa chama cha Kiisilam kinachotawala nchini Tunisia, Ennahda, amesema wamekubaliana kukabidhi wizara muhimu kwa wagombea binafsi, makubaliano ambayo wanafikiri yataharakisha uundwaji wa serikali mpya na kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Kufuatia madai kutoka kwa washirika wao, Rached Ghannouchi amesema chama chake, hakitaongoza wizara za mambo ya ndani, sheria, mambo ya nje na wizara ya ulinzi.

Amesema wizara katika baraza jipya la mawaziri zitasimamiwa na vyama vitano.

Waziri wa mambo ya ndani ametakiwa kuunda serikali mpya kufuatia kujiuzulu kwa waziri mkuu Hamadi Jebali wiki iliyopita.