Waasi 20 wa Boko Haram wauawa Nigeria

Image caption Maafisa wa polisi

Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa limewauwa wapiganaji 20 wa kundi la Kiislam la Boko Haram katika jimbo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo la Borno.

Msemaji wa jeshi amesema kuwa wapiganaji hao waliuawa walipokuwa wakijaribu kushambulia kituo cha kijeshi.

Walidhibitiwa vilivyo na wanajeshi. Silaha na risasi pia zilipatikana. Lakini msemaji wa jeshi hakusema lolote kuhusu maafa.

Kundi la Boko Haram limelaumiwa kwa kufanya mashambulizi kadhaa makali huko kaskazini mwa Nigeria kwa miaka kadhaa sasa.

Mazungumzo

Lakini kikundi hicho hakijasema lolote kuhusu shambulizi hili huko Monguno, takriban kilometa 200 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo, Maiduguri.

Kiongozi wa kundi hilo, Abubakar Shekau, kwa upande mwingine amekanusha madai kwamba kinafanya mazungumzo ya amani na serikali.

Boko Haram yasema kwamba inapigana ili kuunda serikali ya Kiisilamu katika eneo hilo la kaskazini lenye Waisilamu wengi.

Kundi hilo limelaumiwa kwa mauaji ya takriban watu 1,400 people nchini humo.