Pakistan: Karachi yaomboleza mlipuko

Image caption Waokoaji wakijaribu kuzima moto baada ya mlipuko

Mji mkuu wa Pakistan, Karachi, unaomboleza vifo vya watu 45 waliofariki baada ya bomu kulipuka katika eneo lenye Washia wengi.

Zaidi ya watu 150 walijeruhiwa katika mlipuko huo.

Mashule na biashara vilifungwa leo baada ya mgomo kuitwa na vyama kadhaa vya kisiasa ili kuupinga mlipuko huo.

Hakuna kikundi chochote ambacho kimesema kilitega bomu hilo, lililolipuka karibu na msikiti wakati waumini walipokuwa wakielekea makwao baada ya swala ya joini.

Washia walio wachache nchini Pakistan hushambuliwa mara kwa mara na wa wapiganaji wa Kisunni.

Mlipuko huo wa Jumapili usiku uliharibu majumba kadhaa, na kuwasha mioto kwingine, huku umeme ukikatika katika maeneo fulani.

Polisi wanachunguza iwapo lilikuwa shambulizi ya utoaji mhanga.

Waisilamu nchini humo wamegawanyika mara mbili, Washia and Wasunni, na hutofautiana kuhusu maadili, sheria, na usimamizi wa kidini.

Vikundi vya Kishia vimetangaza siku tatu za maombolezi.