Huwezi kusikiliza tena

Kampuni ya Microsoft matatani

Kampuni ya Microsoft imetozwa faini ya dola milioni 731 kwa kukosa kuwapa watumiaji wa programu ya Windows uwezo wa kuchagua mfumo wa kutumia Internet badala ya kutumia mfumo wake wa Internet Explorer moja kwa moja. Kamishna wa ushindani wa kibiashara barani Ulaya alisema kuwa alitaka kuzuia makampuni mengine kukosa kutiza ahadi zao.