Hukumu kuhusu tukio la Port Said Misri

Image caption Maombolezi ya waliouawa katika ghasia za Port Said

Mahakama moja katika mji mkuu wa Misri Cairo, inatarajiwa kutoa maamuzi kuhusu kundi moja la watu wanaotuhumiwa kushiriki katika ghasia mbaya za kandanda mwaka uliopita katika mji wa Port said.

Hukumu za kifo zilizotolewa kwa kundi lingine mwezi Januari pia zinatarajiwa kuthibitishwa.

Zaidi ya watu sabini waliuwawa katika machafuko hao kwenye uwanja wa kandanda, wengi wao wakiwa mashabiki wa timu iliyokuwa ikizuru uwanja huo ya Al-Ahly

Kumekuwa na makabiliano ya siku kadhaa katika eneo la Port Said kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa.

Polisi, wameondolewa kutoka makao yao makuu mjini humo na sasa jeshi linadhibiti jengo hilo.