Odinga afikisha malalamiko mahakamani

Bwana Raila Odinga

Polisi mjini Nairobi, Kenya, wamefyatua moshi wa kutoza machozi kuwatawanya mamia ya wafuasi wa Waziri Mkuu Raila Odinga, nje ya mahakama makuu.

Mawakili wa Bwana Odinga waliwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mapema mwezi huu, ambapo Bwana Odinga alishindwa kwa kura elfu chache na Bwana Uhuru Kenyatta.

Hapo awali Bwana Odinga aliwasihi wafuasi wake wasijihusishe na vurugu.

Mawakili wa Bwana Odinga wamekwenda mahakamani wakidai kuwa kumepita udanganyifu kwenye uchaguzi.