Mwanajeshi wa Ufaransa auwawa Mali

Wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali

Ufaransa imetangaza kuwa mwanajeshi wake mwengine ameuwawa kwenye mripuko kaskazini mwa Mali.

Huku nyuma mawaziri wa nchi za kanda hiyo wamekutana mjini Nouakchott, Mauritania, kujadili swala la Mali wakiwa pamoja na waakilishi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na Umoja wa Ulaya.

Mwanajeshi huyo aliyeuwawa ni askari wa tano wa Ufaransa kufa kwenye vita dhidi ya wapiganaji.