Kiongozi wa dini kati ya waliokufa Syria

Image caption Kiongozi wa dini kati ya waliouawa Syria

Kiongozi maarufu wa Sunni ambaye amekuwa akiunga mkono serikali ya Syria ni mmoja wa watu waliouawa kwenye mlipuko wa bomu uliotokea katika msikiti katikati mwa Damascus.

Mohammed al-Bouti alikuwa mmoja kati ya watu zaidi ya arobaini waliofariki kwenye mlipuko huo.

Kulingana na shirika la utangazaji la Syria, kitendo hicho kilikuwa cha kigaidi na kimetekelezwa na mlipuaji wa kujitolea mhanga katika msikiti wa Iman.

Dr al-Bouti alikuwa amekashifu vitendo vya makundi ya upinzani nchini Syria.

Shirika la utangazaji la Syria lilionyesha waokoaji wakibeba maiti pamoja na waliojeruhiwa kutoka kwenye msikiti.

Kwenye ujumbe wake, kiongozi huyo aliwasisitizia raia wa Syria kuunga mkono serikali katika juhudi zake za kupambana na waasi.